STORY-PENZI LA MSHUMAA MTUNZI-MZIRAY F.M. SEHEMU YA 22








HABARI:
TAKE ONE yafungiwa
Source:JamiiForums
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema Mapunda.

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

Tanzania imeanzisha programu ya simu ambayo inachunguza saratani ya kizazi
Image captionTanzania imeanzisha programu ya simu ambayo inachunguza saratani ya kizazi


HABARI:
Tanzania kuchunguza saratani ya kizazi kwa simu
Source:BBC
Watafiti kaskazini mwa Tanzania wametengeza programu ambayo wauguzi na madaktari wanaweza kuitumia kuchunguza saratani ya kizazi miongoni mwa wanawake ,ambayo wanasema ni ya kwanza na ya kipekee duniani.
Inahitaji madkatari kupiga picha mfuko wa uzazi na simu aina ya smartphone na baadaye kutuma picha hiyo kwa kutumia programu hiyo kwa mtaalam wa matibabu katika kliniki maalum.
Daktari katika kliniki hiyo watachunguza picha hiyo na bila kupoteza wakati kutuma tiba kupitia programu hiyo kwa mfanyikazi huyo wa kiafya akitoa maelezo kuhusu tiba hiyo.

Programu ya simu inayochunguza saratani ya kizazi yazinduliwa
Image captionProgramu ya simu inayochunguza saratani ya kizazi yazinduliwa

Ijapokuwa kuna tataizo ya mawasiliano ya simu,programu hiyo inaruhusu wafanyikazi hao wa kiafya kupiga picha hizo na kuzihifadhi kabla ya kuzituma baadaye.
Nchini Tanzania,zaidi ya wanawake 4000 hufariki kila mwaka kutokana na saratani ya mfuko wa uzazi ,kulingana na shirika la afya duniani WHO.
Saratani ya uzazi inaweza kuzuiwa.
HABARI:
Mkataba wa Nyuklia kati ya Urusi na Marekani wafutwa.
Source:BBC
Urusi imesitisha mkataba wake na Marekani kuhusu kutupwa kwa madini ya ziada ya plutonium ambayo yanaweza kutumiwa kuunda silaha, ishara ya kudorora kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye ushawishi mkubwa duniani.
Kupitia agizo rasmi, Rais Vladimir Putin ameituhumu Marekani kwa kuunda "kikwazo cha kutishia utathabiti, kwa kuchukua hatua zisizo za kirafiki" dhidi ya Urusi.
Bw Putin alisema Urusi imelazimika kuchukua "hatua za dharura kulinda usalama wa taifa la muungano la Urusi".
Moscow imetoa masharti ya kutimizwa na Marekani kabla ya kurejelewa kwa mkataba huo.
Chini ya mwafaka huo wa mwaka 2000, kila taifa linapaswa kuangamiza tani 34 za madini ya plutonium kwa kuyachoma kwenye vinu vyake.
Mpango huo ni sehemu ya juhudi za kimataifa za kupunguza silaha za nyuklia.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema tani 68 za madini ya plutonium ambazo zingeangamizwa "zinatosha kuunda silaha 17,000 za nyuklia".
Pande zote mbili zilikuwa zimetia saini upya mkataba huo mwaka 2010.
Kwingineko, Marekani nayo imetangaza kwamba itasitisha mazungumzo na Urusi kuhusu mzozo Syria.
Marekani imesema Urusi haijatimiza masharti yaliyoafikiwa chini ya mpango wa kusitisha mapigano kwa muda mwezi jana, ambao umesambaratika.
Urusi imesema hatua hiyo ni ya kusikitisha na badala yake ikailaumu Marekani kwa kujaribu kuiwekea lawama Urusi.

Vladimir PutinImage copyrightREUTERS
Image captionBw Putin ameweka masharti kabla ya mkataba huo kurejelewa

Bw Putin aliwasilisha mswada kwa bunge la taifa hilo ambao unaeleza masharti yanayofaa kutimizwa na Marekani kabla ya kurejelewa kwa mkataba huo wa madini ya plutonium.
Masharti hayo ni pamoja na:
  • Kupunguzwa kwa wanajeshi wa Marekani na silaha zake katika nchi zilizojiunga na Nato baada ya 1 Septemba 2000
  • Kuondolewa kwa vikwazo vyote vya Marekani dhidi ya Urusi na kulipwa fidia kutokana na madhara yaliyotokana na vikwazo hivyo.
Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya waliiwekea Urusi vikwazo kufuatia hatua ya Moscow ya kuchukua jimbo la Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014, pamoja na hatua ya Urusi ya kuunga mkono wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa maeneo ya mashariki kwa Ukraine.
MICHEZO
Song apata fahamu
Source:BBC
Aliyekuwa nahodha wa kikosi cha soka nchini Cameroon Rogobert Song hatimaye amepata fahamu ,kulingana na mamlaka.
Beki huyo wa zamani wa timu ya Liverpool na West Ham sasa ameanza kupumua bila ya usaidizi ,siku mbili baada ya kukimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi.
Song mwenye umri wa miaka 40 alilazwa katika hospitali ya Younde siku ya Jumapili baada ya kupoteza fahamu.
Mchezaji huyo ambaye ni shujaa wa kitaifa nchini Cameroon ,alilishindia taifa lake vikombe viwili vya bara Afrika na kushiriki katika michuano minne ya fainali za kombe la dunia
Alitarajiwa kusafirishwa hadi mjini Paris kwa matibabu zaidi chini ya agizo la rais wa Cameroon Paul Biya.
"Baada ya rais kuelezewa ,alitoa agizo kwa wizara ya afya kufanya kila iwezalo ili kumsafirishwa ng'ambo'' ,alisema msemaji wa serikali Issa Thsiroma.
''Tunashukuru vifaa vya hali ya juu vya matibabu na utaalam tulionao nchini Cameroon,tumefanikiwa kudhibiti hali yake,ili aweze kusafirishwa'',aliongezea msemaji huyo.