HABARI:

Trafki afutwa kazi kwa kula Rushwa Zanzibar
Source:JamiiForums
Jeshi la Polisi Zanzibar limemkamata askari wa jeshi hilo anayetuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni kufuatia picha ya video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni.Uamuzi wa kukamatwa askari huyo ulitolewa na Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar, CP Hamdan Omar Makame na kuelezea masikitiko makubwa ya jeshi hilo kutokana na kitendo hicho cha aibu na kinacholitia doa jeshi hilo.Katika video hiyo, askari huyo anaonekana akihimiza kupewa rushwa baada ya kuwakamata raia hao wa kigeni kwa dereva wa gari walilokuwemo akiwa hajafunga mkanda na kuchukua leseni yake na kumhakikishia kuwa aendelee na safari kwani atamlinda na kuonekana akipokea rushwa hiyo.Amemtaja askari huyo kuwa ni Sajenti Talib Hamad na sio Alu huku pia akidai kuwa kitendo hicho kilifanyika Mkokotoni na sio Mahonda kama alivyokaririwa asakari huyo katika video hiyo.CP Makame ametoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo katika kufichua maovu na kudai kuwa ikithuibitika polisi huyo amekiuka taratibu za kipolisi na kuwepo kosa la jinai atapelekwa katika vyombo vya sheria vya dola.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »