Unknown 02:26 Unknown STORY-PENZI LA MSHUMAA MTUNZI-MZIRAY F.M. SEHEMU YA 21 Ilipoishia sehemu ya 20 “We unashangaa kumtoa Tanga kumleta Dar,anasema na familia anahudumia,upo hapo?”Brenda naye akatoa jibu la kejeli. “Au mwenzetu ana mtoto katika familia hiyo?” “Mwenzangu mmmh!hebu tuyaache hayo tusije tukampa homa Vivian wa watu bure!Kwanza hapo alipo ana mawazo chungu nzima juu ya lishuga mami la Denis.” “Mmemaliza?”Denis aliwahoji wadogo zake waliokuwa wanamjadili kwa mipasho. Sasa endelea.... “Utajua mwenyewe kama ndiyo tumemaliza au ndiyo tunaanza.”Brenda alijibu huku akiwa anabinua midomo yake kwa jeuri.Baada ya Denis kupewa jibu hilo,aliinuka na kutoka zake nje kisha akaingia ndani ya gari la kuliwasha. “Denis!we Denis unakwenda wapi sasa wakati hatujamaliza haya mambo?”Mzee Mwamba alikazana kumwita Denis bila mafanikio. “Denis mwanangu rudi kwanza tuyamalize.Mnaona sasa mlichomfanyia kaka yenu?”Bi Asma aliwashambulia mabinti zake. “Heee!mama na wewe unahangaika na mtu mzima wa nini!Mwache aende zake.Kwahiyo asiambiwe ukweli au?Atajibeba kwa mbeleko ama mikono.”Brenda aliendelea kudhihirisha jeuri aliyokuwa nayo mbele ya wazazi wake. Denis aliwasha gari na kukanyaga mafuta huyoo akaelekea zake Mikocheni nyumbani kwake.Alimpigia simu Dick na kumweleza hali halisi na kumwomba wakutane Muhimbili.Baada ya kuongea na Dick alimpigia Vivian ili ajaribu kumfahamisha zaidi juu ya maamuzi yake ya kumsaidia Shaimaa.Alipiga simu ikaita weee!bila kupokelwa.Alijaribu tena na tena lakini hali ikawa vile vile. Mara ya mwosho alipopiga alikutana na sauti ya mdada toka huduma kwa wateja ikimtaarifu kuwa namba anayopiga kwa muda huo haipatikani labda ajaribu tena baadae.Denis alitupa simu yake kwenye meza kisha akajilaza kitandani.Mawazo chungu nzima yalizunguka ndani ya kichwa chake akitafakari hatma ya penzi lake.Kutokana na hilo hakufanikiwa kupata hata lepe la usingizi.Palipokucha tu Denis alijiandaa na kuanza safari ya kuelekea Muhimbili hospitali. Alipofika maeneo ya Fire alimpigia simu Bi Asma akawa hapatikani.Hakujali sana,alikanyaga mafuta na kukunja kushoto kisha akaiacha shule ya sekondari Azania na kusonga mbele.Aliingia Muhimbili hospitali majira ya saa nne na nusu asubuhi.Alishangaa kuambiwa kuwa mgonjwa wake hajala kitu chochote tangu jua lilipochomoza.Jambo hilo lilimsikitisha sana wakati pesa ya matumizi alishampa mama yake Shaimaa kwaaajili ya kumhudumia mwanaye kwenye masuala ya chakula na mambo mengine. Alitoa tena simu yake mfukoni na kumpigia mama huyo lakini namba yake ikawa bado haipatikani.Aliamua kuchukua uamuzi wa kwenda kumnunulia mgonjwa wake vyakula laini laini vya kuipoza njaa yake.Baada ya Shaimaa kushiba Denis alianza kuzungumza naye taratibu. “Vipi hali yako unaionaje?” “Kwa kweli hali yangu namshukuru Mungu siyo mbaya sana.Ila leo asubuhi dokta alikuja kunipima tena hivyo nasubiria majibu kabla ya kuanza matibabu.”Shaimaa alizungumza kwa sauti ya upole.Uso wake uligoma katakata kuificha aibu aliyokuwa nayo kutokana na mambo aliyomfanyia Denis.Roho yake ilimsuta na kumsuta.Alitaka kuomba msamaha lakini akasita.Machozi yalianza kumtiririka kama maji. “Basi usilie Shaimaa utajiongezea maumivu.Usijali,utapona tu na kurudi katika hali yako ya kawaida.”Denis alikuwa mbembelezaji wa kilio kile. “Yaani sijui hata nikushuru vipi kaka yangu.” “Usijali Shaimaa,haya ni mambo ya kawaida tu.” “Mama yupo wapi?”Shaimaa alimuulizia Bi Zena baada ya kutomtia machoni tangu walipoachana jana yake. “Mama nimejaribu kumpigia simu lakini hapatikani.Ila nadhani bado yupo hotelini,nitakwenda kumcheki muda si mrefu.”Wakati wakiendelea na mazungumzo,mara mlango wa ile hodi ukafunguliwa. “Mr Denis.” “Naam dokta.” “Njoo ofisini mara moja.” “Sawa dokta nakuja sasa hivi.”Denis alihitajika kwenye chumba cha daktari kwa mazungumzo kadhaa. “Ngoja nikamuone dokta halafu nikitoka hapo nimfuate mama.”Denis alimuaga Shaimaa. “Denis.”Shaimaa aliita huku akilengwa lengwa na machozi. “Naam.” “Mwenyezi Mungu akubariki sana.” “Usijali Shaimaa tupo pamoja.”Denis alipoingia kwa daktari alikumbana na taarifa iliyomuumiza zaidi moyo wake. Dokta alimwambia kuwa mifupa ya miguu ya Shaimaa ilivunja vibaya sana hivyo uwezekano wa kuiunga ni mgumu mno.Ili kunusuru maisha ya binti huyo wameona ni heri waikate miguu yote miwili kumwondolea uwezekano wa kupooza maisha yake yote.Denis alisikitishwa mno na taarifa hiyo.Alitafakari jinsi msichana huyo alivyokuwa muhimili wa familia yao halafu leo ndiyo awe mlemavu wa kudumu!Jambo hilo lilimletea sononeko la moyo. Kwa kweli Denis lipata uchungu wa hali ya juu hadi akafikia hatua ya kudondosha chozi mbele ya daktari.Dokta alitumia muda mwingi kumbembeleza kijana huyo ambaye hakuwa na uhusiano wowote ule na Shaimaa na wala hakuwahi kumwona hata siku moja zaidi ya siku ile ya ajali tu.Baada ya Denis kutulia aliamua kutoka nje na kukaa kwenye viti vya mapumziko. “Denis vipi,mbona umeshika tama?Unaumwa au?”Denis alikurupuka toka kwenye lindi la mawazo na kumtazama aliyemgusa begani na kumuuliza kulikoni.Baada ya kuziona sura za Dick na Dolan machozi yakaanza kumtoka upya. “Denis unalia nini?Kwani kuna tatizo gani hebu tuweke wazi?”Dolan alimsisitiza Denis aeleze ukweli juu ya kile kinachomsumbua.Denis hakusita kuwapa maelezo aliyopewa na daktari wa mifupa wa pale Muhimbili juu ya tatizo la Shaimaa. “Haa!yaani Denis sisi tulifikiri pengine baba yako ama mama kafariki kumbe unamlilia huyo mwanamke muhuni aliyekuingiza matatizoni bila hatia.” “Daah!halafu Denis mambo yako yanachekesha sana.Hivi upo sawa kweli?”Tofauti na matarajio yake,Denis alishangazwa sana na mapokezi ya rafiki zake juu ya jambo lile. “Kwahiyo hilo siyo jambo la kuhuzunisha?”Denis alihoji. “Hata kidogo,kwasababu wewe siyo uliyemgonga wala huna uhusiano wowote na huyo binti.” “Ni kweli Denis,anachokisema Dolan yupo sahihi kabisa.Hupaswi kumsikitikia mtu ambaye hakuwa na hata chembe ya aibu kwa kukusingizia jambo kubwa kama lile mpaka ukawekwa ndani kwasababu yake.Suala hilo haliingii akilini hata kidogo.”Hakuna aliyekuwa upande wa Denis. “Mnajua ni kwanini alinisingizia kesi hiyo?”Denis alihoji. “Sisi hatujui,kwani tulikuwepo?Wewe ndiyo unafahamu kila kitu.Au labda pengine unajuana na huyo msichana siku nyingi halafu unatuzuga.” “Hata!mimi simfahamu hata kidogo na wala sijawahi kumwona mahali popote pale.Hatuwezi kujua ni kwanini alinisingizia hili suala.Nadhani akipona ndiyo itakuwa muda muafaka wa kumhoji na kuujua ukweli.” “Ehe!kwahiyo umeamuaje juu ya tatizo lake?”Dolan alimtupia Denis swali hilo la mtego. “Mmmh!hapo ndipo pagumu.Daah!yaani binti wa watu akatwe miguu wakati yeye ndiyo mhimili wa familia yao.” “Mhimili wa familia yao!kivipi?”Dick alishtushwa kidogo na kauli ya Denis.Denis aliwaleza rafiki zake hali halisi ya familia ya Shaimaa na jinsi binti huyo alivyokuwa tegemeo la familia hiyo.Maelezo hayo yalimsikitisha kila mmoja hatimaye wakadondosha nyuso zao chini kwa huzuni. “Masikini!kumbe familia yao ina maisha magumu namna hiyo!Duuuh!sasa sijui hapo tunafanyaje?” “We acha tu,huo mtihani ndugu yangu.” “Kwahiyo Denis dokta amesema hakuna uwezekano wowote ule wa kuiunga miguu ya binti huyo?”Dick aliuliza. “Kwa maelezo ya dokta inaonesha kabisa wameshakata tamaa ya kuwepo kwa uwezekano huo.”Denis alieleza. “Hata hospitali za nje ya nchi?” “Mmmh!sijui kwa kweli.Ila pia nilikuwa na wazo hilo lakini nimeshindwa kuelewa ni nchi gani ya kumpeleka.” “Labda Uingereza ama India.Nadhani huko kuna wataalamu wazuri zaidi pamoja na vifaa vya kisasa vya matibabu.”Dick alishauri. “India ndiyo pazuri zaidi ila nahofia gharama zake.”Dolan naye alitoa mchango wake wa mawazo juu ya tatizo hilo. “Gharama si tatizo kaka.Hizi pesa tunazitafuta ili tuzitumie.Hii dunia tunapia tu,naweza nikafa leo nikaacha kila kitu.Sasa nitakuwa nimepata faida gani kama sitowasaidia watu masikini kama hawa?”Denis aliingiliwa na malaika wa huruma na kumjaza moyo wa utoaji hivyo akawa radhi kumsaidia Shaimaa kwa hali na mali.Aliingia kwa daktari na kumweleza wazo la kumpeleka binti huyo nje ya nchi kwa matibabu zaidi.Dokta alimwambia uwezekano huo upo kwa hospitali za nchi zilizoendelea. Denis alitoka chumba cha daktari akiwa na tabasamu nono kinywani mwake.Aliwachukua wenzake wakaingia hodini alipolazwa Shaimaa na kumjulia hali.Binti huyo alifarijika sana kutokana na upendo alioupata toka kwa Denis na marafiki zake.Walimtia moyo kwa kumpa tumaini juu ya maisha yake. Hata hivyo hawakumueleza jinsi tatizo lake lilivyokuwa kubwa kiasi cha kutakiwa kupelekwa nje kwa matibabu ya kina zaidi.Waliamua kumficha kwanza ili wasije wakampa presha na maradhi ya moyo bure!Wakati mazungumzo yakiendelea mara simu ya Denis ikaita.Alipotazama juu ya kioo cha simu aliliona jina la mchumba wake. “Nitakupigia baadae sasa hivi nipo hospitali.”Denis alipopokea tu simu bila hata salamu alimweleza hayo Vivian kisha akakata simu.Alijumuika na wenzake kuendelea kubadilishana mawazo na mgonjwa. “Denis.”Shaimaa aliita. “Naam.” “Ulisema utamfuata mama,yupo wapi?” “Oooh!samahani,nilipotoka nilikutana na hawa marafiki zangu tukawa tunapiga stori mbili tatu hapo nje.Kwa kuwa sasa hivi tunaelekea ofisini tutampitia hapo hotelini nimwambie aje kukuona.”Denis na wenzake waliagana na Shaimaa kisha wakatoka nje ya hospitali ile.Denis aliingia kwenye gari lake na akina Dick nao wakaingia kwenye gari walilokuja nalo.Waliondoka kwa mwendo wa taratibu kuelekea katika hoteli aliyofikia Bi Zena.Denis ndiyo alikuwa kiongozi wa msafara huo na kabla hajaingia kwenye geti la hoteli hiyo mara simu yake ikaingia meseji.Aliingiza gari na kupaki kisha akaufungua ule ujumbe mfupi wa maneno ambao ulitoka kwa Vivian. “Nashukuru sana Denis kwa yote unayonifanyia.Yaani unanikatia simu kwasababu ya huyo malaya wako wa Kitanga!Unajifanya humfahamu kumbe ni msichana wako wa siku nyingi.Umeamua kula kuku na mayai yake siyo!Sitaki tena kuumizwa na sasa naachia ngazi.Endelea na maisha yako na mimi niendelee na maisha yangu.Usinipigie simu wala usinitumie meseji.Huu ndio mwisho wa mapenzi yangu na wewe.Ni heri nitafute mtu mwenye kunijali na mwenye mapenzi ya dhati kwangu.Shika hamsini zako na mimi nishike zangu.Kwaheri baba nakutakia maisha mema.Ila nakushauri usisahau kutumia kinga magonjwa ni mengi.” Denis alishusha pumzi ndefu baada ya kumaliza meseji hiyo yenye ujumbe mzito toka kwa mchumba wake Vivian.Mawazo kibao yalivurugana ndani ya ubongo wake na kumfanya ahisi joto lililopitiliza ukizingatia ndani ya gari kulikuwa na Air Condition(AC).Denis alimpenda sana Vivian na wala hakuwa tayari kumpoteza msichana huyo kirahisi namna hiyo.Alitafuta namba yake na kubofya kitufe cha kupigia kisha akaiweka simu sikioni.Simu iliita ikakata,akaamua kupiga tena.Safari hii iliita wee kisha ikakatwa.Alipopiga tena ikawa haipatikani.Aliupiga usukani wa gari kwa mikono yake mara tatu kwa hasira halafu akaukumbatia. ******** Itaendelea.....Asante kwa ufuatiliaji wako wa hadithi hii na Mungu akubariki sana.Nakutakia siku njema yenye mafanikio tele kwako. ******* Kwa maoni au ushauri napatikana kwa namba 0655089197/0766123623 Author : Unknown Share this Related Posts