Muuaji wa madereva bodaboda akamatwa huko Songea mkoani Ruvuma
Source:JamiiForum
Anayedaiwa kuwa kinara wa mauaji ya madereva bodaboda Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Pengo Majuto ambaye aliyetafutwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma kwa Zaidi ya miezi minne sasa amekamatwa akiwa Njombe na kurejeshwa mkoani Ruvuma ili afunguliwe mashitaka yanayomkabili,hatua ambayo madereva bodaboda wamelipongeza Jeshi la polisi kwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wao.
Akiongea na madereva bodaboda katika semina ya usalama barabarani mkuu wa kikosi hicho mkoa wa Ruvuma Abel Swai amewataka madereva hao kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wanafanya kazi zao na kuwatoa mashaka kuwa mtuhumiwa waliyekuwa wakimshutumu kuwa ndiye muaji wao amesha kamatwa na yupo gereza la mahabusu Songea uchunguzi utakapo kamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zitakazo mkabili.
Wakati mtuhumiwa akiwa kwenye gari la polisi mara baada ya kuwasili mjini songea katika standi kuu ya mabasi akitokea mkoani Njombe madereva bodaboda walipomwona walilishambulia gari la polisi kwa kupiga mawe kwa lengo la kutaka kumchukua mtuhumiwa kwa nguvu kwa madai kuwa hata kama amekamatwa ataachiwahuru huru kama ilivyo kuwa siku za nyuma polisi wamewatoa mashaka na kuwahakikishia sheria itachukua mkondo wake.
Nao baadhi ya madereva bodaboda wamelishukuru jeshi la polisi kwa jitihada walizozifanya za kuhakikisha mtuhumiwawao amekamatwa na kwamba wapo tayari kutoa ushirikiano dhidi ya jeshi hilo.
Miezi michache iliyopita kulikuwa na wimbi kubwa la mauaji ya madereva bodaboda ambapo Zaidi ya madereva wanane waliuwawa katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Songea jambo lililozua taharuki kwa wananchi mjini hapa.