Kimbunga cha Matthew
Image captionKimbunga cha Matthew

HABARI:
Kimbunga chashambulia Haiti
Source:BBC
Kimbunga Matthew kimeharibu miundombinu muhimu kama vile barabara ambapo maafisa wanasema kuanguka kwa daraja kumegawa sehemu ya kusini na sehemu nyengine ya nchi.

Eneo lililopigwa na kimbunga Haiti
Image captionEneo lililopigwa na kimbunga Haiti

Mtu mmoja mpaka sasa amepoteza maisha nchini Haiti na wengine wanne kutoka nchi jirani ya Jamuhuri ya Dominica.
Bado mpaka sasa haijafahamika kiwango cha uharibifu wa kimbunga hicho nchini Haiti, lakini nyumba nyingi zimebomolewa, huku barabara zikiwa hazipitiki kutokana na miti iliyoanguka pamoja na mafuriko.

Maji yakitiririka Port-au-Prince
Image captionMaji yakitiririka Port-au-Prince

Wahanga wa kimbunga hicho wanaendelea kujaa katika makazi yaliyotengwa na serikali katika mji mkuu wa Port-au-Prince huku mamlaka ikiendelea kuomba msaada wa maji pamoja na chakula.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »